WANANCHI 520 WAHUDUMIWA SIKU YA KWANZA NA MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA MKOANI MBEYA
Posted on: May 5th, 2025
Zaidi ya wananchi miatano ishirini wamehudumiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya ndani ya siku moja ya ufunguzi wa kambi hiyo hapo jana Mei, 5 2025.
Wananchi hao wamenufaika na mpango wa Mhe. Rais Dkt. Samia unaolenga kusogeza huduma za kibingwa na ubingwa bobezi karibu na wananchi, pamoja na kuwajengea uwezo watumishi waliopo ngazi mbalimbali za utoaji huduma katika Hospitali mbalimbali hapa nchini.
Akitoa ripoti leo asubuhi, Mratibu wa Huduma za Kliniki, Mbeya RRH, Dkt. Mwakyusa amesema zaidi ya wananchi 520, wamepatiwa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi, ambapo wengine leo Mei 6, wamefanyiwa huduma za upasuaji wa kibingwa.
Katika Kambi ya Madaktari Bingwa na Bingwa Bobezi ambao wameweka kambi Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mbeya wanahudumia wananchi kwa Ubingwa na ubingwa Bobezi kwenye maeneo kama vile; Magonjwa ya Moyo ,magonjwa ya Figo, upasuaji Rekebishi,upasuaji wa ubongo ,Mfumo wa mkojo,magonjwa ya saratani ,upasuaji wa Macho ,afya ya akili ,upasuaji wa Sikio, Pua na Koo ,Upasuajiwamifupa,UpasuajiwaJumla,Upasuaji wa Kinywa na Meno ,Matibabu ya Watoto Magonjwa ya Wanawake na uzazi ,Huduma za Tiba ya viungo na utengamao
Malengo mahususi ya Serikali kupitia Wizara ya Afya ni kuimarisha afya za Wananchi na kuhakikisha kila Mtanzania anapata matibabu stahiki bila kikwazo cha kufuata huduma za kibingwa mbali na maeneo yao